Hili ndio eneo lijulikanalo kama MEGIDO hapa ndio patakapokuwa uwanja wa mapambano wa vita ile kuu, na ya mwisho, kulingana na unabii wa kibiblia, moja ya siku hizi patageuka na kuwa bafu la damu. Hapa ndipo mahali vita ya tatu na ya mwisho ya duniani itakapopigwana ijulikanayo kama HAR-MAGEDONI (Ufunuo 16:16), pale mataifa yote ulimwengu, yakiongozwa na mataifa kutoka maawio ya jua, yatakapokusanyika ili kujaribu kuisambaratisha Israeli katika uso wa dunia, Na sasa mipango yote ipo wazi, kwa jinsi tunavyoona idadi ya mataifa yanayoichukia Israeli kuzidi kupanda kwa kasi. Hii Inatupa Rai sisi kama bibi-arusi kunyanyua vichwa vyetu na kusema wokovu wetu umekaribia.. Kwani mpaka hayo yatokee kanisa litakuwa tayari limeshanyakuliwa..…..Swali ni kwako ambaye upo katika mawazo mawili?..ambaye hujampa KRISTO maisha yako.
No comments:
Post a Comment