"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Wednesday, May 22, 2019

MWEZI NI ISHARA GANI KWETU?.


Shalom mtu wa Mungu, karibu tujifunze tena maneno ya Mungu.

Kama wengi wetu tunavyojua kuwa, siku ya Bwana inakuja, siku ya hukumu yake ambapo Bwana atauhukumu ulimwengu kwasababu ya ubaya wake..(Isaya 13:11 inasema hivyo)

Na katika siku ya Mwisho,wafu wote watafufuliwa na Kiti cheupe cha Hukumu kitawekwa na Yesu Kristo ataketi juu yake, na kila mtu, mmoja baada ya mwingine atasimama mbele yake atoe hesabu ya mambo yake yote aliyoyafanya tangu siku alipozaliwa mpaka siku aliyokufa, yote hayo yatamulikwa katika kioo kikubwa sana, na kuonekana mbele ya watu wote na hapo ndipo kila mtu atapasa sifa yake, au aibu yake. (1Wakorintho 4:5)

Litaonekana tendo moja baada ya lingine, liovu au la haki litaonekana pale…kama mtu alikuwa ni mwasherati yataonekana matukio yote aliyoyafanya ya uasherati, siku aliofanya, mtu aliyefanya naye, mwaka, mwezi, mpaka dakika na sekunde alizokuwa anafanya…na watu wote wataona hakutakuwa na siri, kama mtu aliyafanya tendo Fulani la haki nalo pia litaonekana mwaka, siku, mpaka sekunde ya tendo hilo. Iwe alifanya kwa siri au kwa wazi yote yatakuwa bayana.

Na ni kwanini Mungu anataka watu wote waone?..Ni kwasababu yeye ni muhukumu wa haki na hivyo asitokee mtu yeyote atakayesema Yule kaonewa au Yule kapendelewa, watu wote watashuhudia matukio ya yaliyokuwa yanaendelea miongoni mwa watu.
Yohana 5: 28 “Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, NA WALE WALIOTENDA MABAYA KWA UFUFUO WA HUKUMU”.
Na Leo kwa Neema za Bwana tutaangalia ni kwa namna gani..MATUKIO(AU MATENDO) YA WANADAMU YANAVYOREKODIWA MBINGUNI.

Unajua unapoingia Benki au kwenye duka Fulani kubwa lenye bidhaa nyingi za thamani huwa wanaweka camera Fulani zizazorekodi matukio yote yanayoendelea kule ndani (CCTV). Wakati mwingine zinawekwa sehemu za kujificha wakati mwingine sehemu za wazi kabisa…

Sasa lengo la kuweka hizi camera kwa wazi ni ili watu wote wazione wanaoingia pale na waliopo kule ndani, ili wajue kuwa mambo yao yote wanayoyafanya yanarekodiwa na hivyo iwatengenezee hofu ya kutaka kujaribu aidha kuiba au kufanya kitendo chochote cha uhalifu. Hilo ndio lengo la hizo camera (CCTV) kuweka wazi. Ni ili mtu anapoingia na kuziona zile aingiwe na hofu ya kutaka kujaribu kufanya tukio lolote ovu..
Na ndivyo hivyo hivyo katika maisha haya…Tunapoingia katika huu ulimwengu Bwana Mungu ameweka camera yake juu inayorekodi mambo yote ya wanadamu tangu tunapozaliwa mpaka tunapokufa..na lengo la kuifanya ionekane ni ili watu waionapo waogope kufanya mambo maovu hapa duniani wakijua kuwa siku moja itaweka bayana matukio yote…Na hiyo camera (au CCTV) Ni huu MWEZI TUNAOUONA! Hapa juu ya vichwa vyetu..Huu mwezi tunaouona haupo tu pale juu kutufurahisha sisi wanadamu hapana! Au kutoa tu mwanga wakati wa usiku…ile ni camera Mungu aliyoiweka ionekane wazi ili watu tuogope kuishi maisha yasiyofaa hapa duniani.. Leo nitakuhakikishia kwanini Mwezi ni Camera ya huu ulimwenguni.

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa mambo ya Sayansi…utakuwa umekutana au umewahi kusikia kitu kinachoitwa SATELLITE ( au satelaiti). Satelaiti ni kifaa cha kisayansi kinachowekwa juu sana (Maili nyingi sana angani)…ambacho kifaa hicho kinawekwa katika mfumo wa kuizunguka dunia kama vile mwezi unavyoizunguka dunia…Na kinakuwa na kazi nyingi tofauti tofauti…Lakini kazi kubwa satelaiti inayofanya ni KUREKODI NA KUPIGA PICHA ZA MATUKIO YANAYOENDELEA DUNIANI.

Kwa kutumia satelaiti mtu anaweza kukuona mpaka hapo ulipo na shughuli unazofanya si hivyo tu Satelaiti pia inauwezo wa kupicha za miji, na mienendo ya watu wengi na shughuli zao…unaweza kuchunguzwa hapo ulipo pasipo wewe kujijua kwa kupitia satellite…na inamatumizi mengine mengi tu.

Sasa wanasayansi walikitengeneza hichi kifaa kwa kujifunza tabia za mwezi, wakatumia fomula ile ile ya jinsi mwezi ulivyo juu na unavyozunguka dunia, wakaitumia na wao pia kupandisha kifaa chao hicho kama MWEZI WAO juu angani. Na kwasababu hiyo MWEZI huu tunaouona sisi wakaupa tafsiri ya kisayansi kuwa NI SATELAITI YA ASILI…Kwahiyo Wanasayansi hawaujui huu mwezi kwa tafsiri nyingine zaidi ya hiyo..wenyewe wanajua kuwa Mwezi ni satelaiti ya asili(kwa kiingereza natural satellite)…na hizo wanazozitengeneza wao wanazijua kama “satelaiti za kutengenezawa (kwa kiingereza artificial satellites)”. Kafuatilie jambo hilo utalielewa zaidi.

Sasa wao wameutafsiri mwezi kama SATELAITI YA ASILI, lakini hawajui kwanini wameutafsiri hivyo.. Lakini sisi Wakristo Bwana katupa macho ya rohoni kujua. Kama wao walitengeneza mwezi wao wa asili na kuupandisha juu sana, na kuzunguka dunia kwa lengo la kurekodi matukio yanayoendelea duniani..kadhalika na huu mwezi wa asili au satelaiti ya asili kama wanavyouita..unafanya kazi hiyo hiyo kama ya kwao…ya kurekodi matukio yote yanayoendelea duniani tena kwa ufasaha zaidi. Ingawa kwa namna ya macho ya kawaida huwezi kulihakiki hilo.

Ndugu yangu…MWEZI NI SATELAITI YETU. … TV unayoitazama matukio unayoyatazama Youtube na internet yote hayo ni kazi ya satellite, sasa hizi wakati mwingine hazina uwezo wa kuchukua kila tukio duniani vizuri…lakini hiyo satellite ya asili iliyotengenezwa na Mungu mwenyewe haina chenga hata kidogo..inarekodi kila kitu hata vile vya sirini.

Ndugu hakuna chochote unachoweza kukificha sasa, Mbingu na Nchi zinarekodi.. huu mwezi ni Jicho la Mungu ambalo kaliweka wazi ili watu wote waone, na wajue kuwa wanatazamwa juu, na waogope kufanya maasi…Waebrania 4:13 “…Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu”….Je! na wewe unaficha dhambi zako? Ni mwasherati kwa siri? Fahamu kuwa matendo yako yanarekodiwa juu, je! Ni mlawiti kwa siri? Mtazamaji wa pornography kwa siri?, ni mfanyaji masturbation kwa siri? Ni mwuaji kwa siri?, mchawi kwa siri? Mwizi kwa siri?...Tambua kwamba hakuna chochote unachoweza kukificha mbele za Mungu…

Siku ile mambo yako yote yatawekwa wazi screen itaonekana mbinguni ukiwa unafanya tukio moja baada ya lingine na utaambiwa ulitolee hesabu na utashindwa na utatupwa katika lile ziwa la Moto, huku moyoni ukijua kabisa umehukumiwa kwa haki…Mgeukie Muumba wako kabla siku za HUU MWEZI KUWA DAMU hazijafika. Kwasababu itafika siku Jua litatiwa giza na mwezi utakuwa mwekundu kama damu…kuashiria mwisho wa kumbukumbu za wanadamu…ndio maana kwenye mbingu mpya na nchi mpya hakutakuwa na MWEZI tena, kwasababu hakutakuwa na kurekodiwa tena kwa matukio ya watu kwasababu watu wote watakuwa wakamilifu.

Biblia Inasema katika Mithali 28: 13 “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. 14 Mwanadamu mwenye kicho yu heri sikuzote; Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara”.

Unaona inasema MSHUPAVU WA MOYO ATAANGUKIA MADHARA, Hayo madhara ni ZIWA LA MOTO

Ufunuo 21: 7 “Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.
Usizifiche dhambi zako leo kwasababu siku moja zitaanikwa mbele ya wote, Tubu leo kwa kukusudia kuziacha kuzifanya, unakusudia kuacha rushwa, ulevi, utukanaji, ulawiti, umalaya, utoaji mimba, uvaaji mbaya, anasa na mambo yote mabaya…Na Bwana atakupokea na kukupa Roho wake mtakatifu atakayekufanya usiwe na hamu ya kufanya hayo mambo tena..ili siku ile ya kutoa hesabu ya mambo yako yaonekane mambo mema tu! Huku

Bwana akubariki sana.

No comments:

Post a Comment