"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Thursday, May 2, 2019

NOTI YA UFALME WA MBINGUNI


Shalom! Mtu wa Mungu karibu tujifunze Neno la Mungu, ambalo ndio Taa yetu ituongozayo uzimani.
 
Jinsi ufalme wa mbinguni unavyotenda kazi, kwa sehemu kubwa sana unafanana na namna ufalme wa duniani unavyotenda kazi, kwahiyo tukiulewa vizuri jinsi ufalme wa duniani unavyotenda kazi, tutauelewa pia vizuri jinsi ufalme wa mbinguni unavyofanya kazi.

Kwamfano katika ufalme wa duniani tunaona kunakuwa na wafalme, na mfalme mkuu, au kunakuwa na Raisi..Kadhalika na ufalme wa mbinguni ni hivyo hivyo, wapo wafalme na yupo mfalme wa wafalme (Yesu Kristo). Na kama vile hukumu za mwisho huwa zinapitishwa na Raisi wa hiyo nchi au Mfalme, na katika ufalme wa mbinguni ni hivyo hivyo hukumu ya Mwisho inapitishwa na Yesu Kristo aliye Mfalme wa wafalme.
 
Lakini pia tunaweza kujifunza katika jambo lingine linalofanyika katika ufalme wa ulimwengu huu, ambalo pia linfanyika katika ufalme wa mbinguni pasipo wengi wetu kulijua. Na jambo hilo si lingine zaidi ya UCHUMI, Yaani mzunguko wa fedha.

Kama wengi wetu tunavyojua, jamii kubwa karibia yote ya wananchi wa Taifa hili wanatafuta FEDHA, kama chombo cha kubadilishana, ili wayafikie mahitaji yao waliyotaka kwa wakati fulani, na kutimiza mipango yao, wengi wanautafuta utajiri kwa nguvu zote, ambao sio jambo baya ni jambo zuri. Na utajiri maana yake ni kuwa na fedha nyingi, kwahiyo tafsiri yake ni kwamba ni lazima mtu atafute fedha nyingi ndio awe tajiri.

Sasa FEDHA NI NINI?.. fedha ni kitu chochote ambacho kimekubaliwa na jamii husika kitumike kama chombo cha kubadilishana huduma au bidhaa,, kinaweza kuwa kuwa karatasi au safaru” na hicho kinakuwa kimepewa heshima ya kubeba THAMANI fulani, mahususi kwa ajili ya kununua kitu chenye thamani ya hiyo fedha…Hivyo Bila kuwa na fedha ni vigumu kupata huduma zile unazozihitaji.

Sasa ukichukua sarafu au NOTI labda tuseme ya shilingi elf 10 au elfu 5 , utagundua kuwa ina pande mbili, upande wa kwanza utaona ina alama fulani fulani hivi, pengine utaona picha zinazozungumzia utajiri wa nchi, au utaona kuna picha ya kiongozi wa nchi mkubwa aliyewahi kupita, au utamaduni wa nchi, na baadhi ya viishara ishara kama nembo ya taifa n.k..huo ni upande wa mbele na upande wa pili wa nyuma..utaona kuna picha za wanyama. Mambo hayo yote yanafunua kuwa fedha ina roho nyuma yake…Ukiipata katika njia sahihi utakuletea mafanikio makubwa kama inavyoonekana katika upande wa mbele, lakini pia usipoipata kwa njia halali, au ukiitumia kwa njia isiyopasa..ina roho ya unyama upande wa pili, itakuharibu badala ya kukujenga…Ndio maana unaona wengine fedha zinawashusha wengine fedha hizo hizo zinawapandisha n.k
 
 

VIvyo hivyo katika Ufalme wa mbinguni kuna UCHUMI, na pia kuna fedha..Na kila mtu ili aweze kudumu katika ufalme wa mbinguni ni lazima awe na fedha za kimbinguni, Na fedha hizo pia zipo katika mfumo wa makaratasi..NA HIZO SIO NYINGINE ZAIDI YA NENO LA MUNGU NDANI YA BIBLIA TAKATIFU. Biblia inasema Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu..(Wakolosai 3:16)..Ina maana kuwa Neno la Mungu ni kama fedha, tunapaswa tuwe nalo kwa wingi ili tuweze kujikimu na mahitaji yetu yote ya rohoni. Ukipungukiwa na Neno la Mungu basi utapungukiwa na mahitaji yote ya kiroho, hutaweza kufanya chochote katika roho ni wazi kuwa kuwa utashambuliwa na matatizo ya kila aina.

Biblia pia inasema katika Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.”..ikiwa na maana kuwa kama vile vile fedha inavyopatikana kwa nguvu na ufalme wa mbinguni ni hivyo hivyo..Wale wote wenye utajiri wa Neno la Mungu mioyoni mwao ndio wanaoteka baraka zote za rohoni, hawababaishwi na mapepo, wachawi, hofu, mashaka au chochote kile kwasababu wameupata utajiri mioyoni mwao.

Na kama vile tulivyojifunza kuwa fedha ina pande mbili, upande mmoja unaelezea utajiri wa nchi, nembo ya nchi, shughuli za kiuchumi za nchi, na nyuso za viongozi wakubwa waliotangulia, kadhalika pia katika NOTI za kimbinguni (yaani Neno lake)..lina pande mbili…Upande mmoja unaelezea Uzuri wa Ufalme wa mbinguni, Mbingu mpya na nchi mpya ilivyo, na pia upande huo huo wa mbele unaonyesha nyuso za viongozi wakubwa waliotangulia..Ndio maana tukisoma Biblia tunaona maisha ya Mitume na Manabii, tunaona mashujaa wa Bwana kama wakina Paulo wakiishindania Imani waliokabidhiwa watakatifu mara moja tu! Hivyo Bwana akaruhusu maisha yao yawekwe kwenye alama ya fedha ya ufalme wa mbinguni Na utaona pia Bwana wetu YESU KRISTO KAMA MFALME WA WAFALME anatokea karibia katika kila Noti, (kila kitabu katika Biblia)..oo haleluya!! Lakini pia sehemu hiyo hiyo ya mbele utaona kunakuwa na Nembo ya nchi, inayoonyesha utamaduni na miiko ya nchi, na katika Biblia (ambayo ndio noti yetu ya kimbinguni) ndani yake tunasoma namna ya kuishi kulingana na utamaduni na utaratibu wa ufalme wa mbinguni.

Lakini pia haiishii hapo, Neno la Mungu (noti ya kimbinguni) inayo upande wa nyuma pia..Ambao huo una picha za wanyama..Kuonyesha kuwa Katika maandiko matakatifu wapo wanyama pia, na kama unavyojua tabia ya wanyama..ni kurarua na kuua, hawana akili..kadhalika katika maandiko matakatifu tunaonywa kuhusu MNYAMA ATAKAYEKUJA KUTOKA BAHARINI, kuwatia CHAPA WALE WOTE, WASIOKUWA NA MUHURI WA MUNGU (soma Ufunuo 13 & 17). Ikifunua kuwa yeyote Yule atakayeupokea ufalme wa mbinguni isivyopaswa ataangamizwa, na kuraruliwa na roho ya Yule mnyama anayetoka kuzimu..Kwahiyo ni kuwa makini sana na fedha hii ya kimbinguni. Ina UTAJIRI, na BADO INA HUKUMU.
Ufunuo 13: 1 “Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.
2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.
3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama Yule”.
Ufunuo 17: 3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu”.
Kwahiyo kwa kujifunza hayo tunaweza kuona ni jinsi gani, tunapaswa tuwe makini sana, tunapoutafuta ufalme wa mbinguni, kwamba tuutafuta kwa njia halali kama tunavyotafuta fedha, ili utupe utajiri wa rohoni, lakini tusipoutafuta kwa njia halali utatuangamiza na tutajikuta tumeangukia chini ya mikono ya Yule mnyama atokaye baharini, na huyo mnyama si mwingine zaidi ya Mpinga-Kristo, ambaye hivi karibuni atanyanyuka…naye atapewa kufanya kazi yake kuwaua wale wote watakaokataa kuipokea chapa ya mnyama. Na mnyama huyo sasa ameshaanza kufanya kazi, na anafanya kazi chini ya Kanisa la Kirumi (Kanisa Katoliki),  sasahivi yupo katika hatua za mwisho mwisho kukusanya madhebebu yote na dini zote ili kuunda Umoja wa dini zote na madhehebu yote, na itafikia wakati mtu yeyote au kanisa lolote likikataaa kuwa mshirika wa umoja huo, litafutiwa usajili, na mtu yeyote atakayekataa kuwa mshirika wa umoja huo hataweza kununua wala kuuza, na hataweza kufanya kazi maana ajira zote zitataka wahusika wawe katika ushirika huo, na yeyote atakayekubali kujiunga na ushirika huo (atakuwa tayari amepokea chapa ya mnyama)..katika usahili wa kuingizwa katika umoja huo vitatumika vitu mbali mbali, kama micro-chips kuingizwa katika mwili…mfumo wa chips utatumika sana sana kwa nchi zilizoendelea, na hizo chips sasahivi zipo tayari, zinasubiri wakati tu wa kuanza kutumika.

Kwa nchi zinazoendelea, sehemu baadhi zitatumika hizo chips lakini sehemu kubwa vitatumika vitambulisho vya kawaida tu, lakini vyenye taarifa zote za dini ya mtu husika, kila mtu atalazimishwa kwenda kuhakiki upya taarifa zake za msingi, na ndani ya kuhakiki huko watalazimishwa wataje ni madhehebu yao au dini zao ambazo zipo kwenye huo umoja..Na endapo mtu atakataa au atakuwa sio mshirika wa mojawapo wa muunganiko huo, ni wazi kuwa hatapata utambulisho huo, hivyo ataonekana ni muhalifu tu! Na hataweza kusafiri wala kwenda popote pale, kazini atafukuzwa, na kadi yake ya benki na ya simu itafungiwa kwasababu hajakamilisha usajili. Jambo hilo litakapoanza dunia yote, itafurahiwa itaonekana ni mfumo mzuri mpya, lakini wengi hawatajua kuwa ndio wanapokea chapa ya mnyama hivyo. Wakati huo unyakuo utakuwa umeshapita! Na kumbuka unyakuo utakuwa ni siri sana, sio wote watajua kuwa unyakuo umepita, hakutatokea ajali mabarabarani kama inavyosemekana, zitasikika habari chache tu za chini chini kwamba baadhi ya watu wametoweka (uvumi fulani tu)…wengi hawataamini kwasababu siku hizi yapo matukio mengi ya watu kutoweka, kwahiyo wengi watajua ni kutoweka kwa kawaida tu! Hivyo watapuuzia, na haitachukuliwa kwa uzito huo.

Baada ya huyo mnyama kumaliza kazi yake ya kuwatia chapa yake wale wote walioachwa kwenye unyakuo, ataanza kuwaua wale waliokataa kusajiliwa kwenye mfumo wake, atatumia nguvu ya serikali, atahimiza serikali zote ziwatoe hao waliokataa kupokea mfumo wao na watu wengi wataonyesha ushirikiano kumpa support huyo mnyama..ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe..kutakuwa hakuna kujificha siku hiyo, baba utaona anamkana wazi wazi mwanae, na kusema huyu mwanangu alikataa kwenda kuhakiki taarifa zake, ana kiburi mkamateni, watakamatwa watu wengi na kupelekwa magerezani na hatimaye kwenye kambi za mateso, sasa hao ndio watasingiziwa kuwa ndio chanzo cha matatizo yote yanayotokea kwenye jamii na duniani, hata kama kulikuwa na mtu ameiba mtaa wa pili, lawama zote watatupiwa hao, wataachwa huru wale wauaji na magaidi, watageukiwa wao, kama vile tu Yesu, alivyofunguliwa Baraba muuaji akasulibiwa yeye. watateswa mateso yasiyokuwa ya kawaida kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu..Ni matezo ambayo hajawahi wala hayataka yatokee.

Ndugu yangu, sio kipindi kizuri hicho kikukute, mimi sitaki kinikute na wewe nakuambia sasa ili nawe kisikukute, kipo karibuni sana kutokea…leo hii itii injili ya Yesu Kristo, Utafute ufalme wa mbinguni kwa bidii zote kama unavyotafuta fedha, maana mwenye nguvu ndio wanaoupata..Anza kujikusanyia utajiri wa kimbinguni kwa kujifunza na kulitii neno lake ambalo ndio Noti yetu. Ndipo utakaposalimika katika dunia hii..
Mithali 2: 1 “Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu;
2 Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu;
3 Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu;
4 Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika;
5 Ndipo utakapofahamu kumcha Bwana, Na kupata kumjua Mungu.
6 Kwa kuwa Bwana huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;”
Usisahau, noti ina pande mbili, na biblia imetupa NJIA mbili za kuchagua kufuata..NJIA YA UZIMA na NJIA YA MAUTI. (Yeremia 21: 8 Nawe waambie watu hawa, Bwana asema hivi, Tazama naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti).

Ni maombi yangu kuwa utachagua njia ya uzima, kama hujampa Bwana Yesu Kristo maisha yako, ndio wakati wakufanya hivyo sasa, usisubiri leo ipite, kwasababu hujui lisaa limoja mbele nini kitatokea, hapo ulipo mwambie Bwana akusamehe makosa yako yote, na mwambie hutaki tena kuishi maisha ya dhambi, na baada ya kuomba sala hiyo, dhamiria ndani ya moyo wako kuacha dhambi kweli kweli, dhamiria kuacha pombe, sigara, rushwa, uasherati, uvaaji mbaya wa vimini na suruali na mapambo ya kidunia hii, dhamiria kuacha kampani mbovu, na mambo mengine yote yasiyofaa..Ukimaanisha kutoka moyoni mwako kuacha hayo mambo, nguvu ya ajabu itashuka juu yako kukusaidia kuyashinda hayo mambo yasikurudie tena…na ukishamaliza hiyo hatua nenda mahali popote wanapoamini ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, ubatizwe hapo, na Bwana mwenyewe atakusaidia kufanya yaliyosalia..

Bwana akubariki sana, tafadhali pia “share” kwa wengine nao waokoke.

No comments:

Post a Comment