"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Tuesday, May 7, 2019

WANA WA MAJOKA.

Kwanini Bwana aliwaita waandishi na mafarisayo wana wa majoka?, Na hao wana wa majoka kwasasa wanawawakilisha watu wa namna gani?.

Najua ulishawahi kuyasoma haya maandiko, lakini naomba usome tena kwa utulivu lipo jambo nataka ulione la tofauti naamini litakufungua macho yako na kukuponya katika uelekeo ambao pengine ulidhani upo sawa kumbe haupo sawa.
Mathayo 23:29 “Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki,
30 na kusema, KAMA SISI TUNGALIKUWAKO ZAMANI ZA “BABA ZETU”, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii.
31 Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii.
32 Kijazeni basi kipimo cha baba zenu.
33 ENYI NYOKA, WANA WA MAJOKA, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?
34 Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;
35 hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu.
36 Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.”
Amen.

Jaribu kufikiria hawa watu kauli waliyokuwa wanaitumia siku zote za maisha yao… KAMA SISI TUNGALIKUWAKO ZAMANI ZA “BABA ZETU”, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii…

Hiyo ni uthibitisho tosha, kutuonyesha kuwa wao walikuwa sio wana wa manabii, sio uzao wa watu waliomcha Bwana, walikuwa na baba zao tofauti na wale tunaowasoma habari zao kwenye biblia, walikuwa tofauti na wakina Musa, tofauti na wakina Samweli, tofauti na wakina Eliya, tofauti na akina Daudi, tofuati na makuhani wote wa kweli wa Mungu..Tunasoma wanaafikiana kabisa kuwa na kuthibitisha kuwa kweli BABA zao walikuwa na huduma moja tu duniani nayo ni hiyo, kama sio kuwapiga watu wa Mungu, na kuwafukuza miji kwa miji basi waliwasulibisha na kuwaua hadharani.

Maneno hayo yakiwa yanatoka katika vinywa vyao kwa ujasiri, tunamwona Bwana Yesu akiwashangaa na kuwauliza,..mwajishuhudia kabisa mkisema kama “sisi tungalikuwako zamani za BABA ZETU!!!....ati nini? …BABA ZETU!!

kumbe wale ni BABA zenu??, Baba zenu nyie sio mitume na manabii waliouliwa na wale wauaji, lakini wale ndio mnaowaona kuwa ni baba zenu..Mnajishughudia kabisa kuwa nyie ni watoto wa wauaji,!! Mnajishuhudia kabisa nyie ni wana wa majoka, mnasubiri kukua mkomae kama baba zenu ili nanyi mfanye kazi zile zile walizokuwa wanazitenda baba zenu za kuwapiga manabii wa Mungu na kuwaua na kuwasulibisha… Kwasababu WANAJISHUHUDIA WENYEWE.

Lakini cha kusikitisha ni kwamba hata leo hii, katika kanisa la Mungu jambo hili hili linajirudia..Leo hii ndugu nataka nikuambie kabla haujapinga neno lolote hapa, au kutoa maneno ya kejeli naomba nikuulize swali BABA ZAKO NI WAKINA NANI?..Unajishuhudia kwa mababa wapi?..Usije ukajikuta na wewe upo miongoni wa watoto wa MAJOKA yaliyowaua mababa wa Kweli wa Mungu, ukijidanganya kuwa wewe nawe ni miongoni mwa wana wa mitume…Jitathimini.

Kabla hajifikiria kusema mimi ni mshirika wa dini Fulani, au dhehebu Fulani embu fanya utafiti kwanza, hao mababa zako au waanzilishi wao walikuwa na historia gani huko nyuma? Chimbuko lao ni lipi?.

Cha kuhuzunisha sana KANISA la kirumi ( KATOLIKI) ambalo leo hii ndio kanisa lenye washirika wengi ulimwenguni, na washirika wake na wengi wa washirika wake wanajivunia kuitwa Wakatoliki, lakini tukilitazama chimbuko lake ni la kushtusha sana, nasema tena sio kidogo, bali ni sanaa!!..Hivi karibuni viongozi wa kanisa hilo likiongozwa na PAPA kiongozi wao mkuu wanaomba msamaha kwa mauaji ya wakristo na watakatifu wengi wa Mungu zaidi ya MILIONI 68 yaliyofanywa tangu kipindi cha kanisa la kwanza hadi wakati wa matengenezo. ..
Wanakiri kuwa ni kweli “BABA” zao walifanya hivyo, na ndio maana wanawaombea msamaha, ..Ingekuwa sio baba zao wasingejisumbua kuwaombea msamaha, lakini sasa wanakiri kuwa Baba zao, ndio waliohusika na mauaji yale mabaya na ya kikatili hawakuwa mitume watakatifu wa Mungu ambao hatujawahi kuona hata siku moja katika maandiko mtume mmoja kamnyooshea mtume mwanzake kidole, sembuse kuua na kusulibisha watakatifu zaidi ya milioni 68, kama sio MAJOKA haya ni NINI tena??. Tuwe wawazi.

Na kibaya zaidi ndugu zetu wengine wasiojua historia ya kanisa vizuri, wanaungana nao na kujiita wao ni watoto wa Kanisa hilo la damu. Hawajui kuwa na wao mbele za Mungu wanaingizwa katika hatia moja na baba zao wanakuwa wana wa majoka.. Ndugu usidhani haya mambo hayafanyiki hata sasa, mimi nakueleza kitu nilichokishuhudia na kukionja mwenyewe, siongei kidini au kishabiki, au kwa chuki, nami pia nilikuwa huko kwa neema za Bwana nikatoka..Kwa ujasiri wote nataka nikuambie Hasira ya Mungu ipo juu ya kanisa hili la uongo KATOLIKI. Ndugu tenga muda usome historia ya kanisa, usikubali tu! Kurithishwa kitu pasipo kujua asili yake..

Na ndio maana Bwana Yesu bila unafki aliwaambia..
32 Kijazeni basi kipimo cha baba zenu.
33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?
34 Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;
35 hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu.
36 Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.”

Usipotaka kutoka huko, katika kanisa la damu, ujue hukumu ipo juu yako, na wewe pia utakuwa umeshiriki katika kuwaangamiza watakatifu wa Mungu bila hata ya wewe kujua, wakati huo kama sio sasa, utadhani unamtolea Mungu Ibada kwa watu wa Mungu kufa, kumbe umeshakomaa kutika viwango vya juu vya baba zako kwa uuaji. Usidhani utagundua, hutagundua hilo mpaka siku ile ya hukumu ndio utajua ni jinsi gani umeshiriki katika damu za watakatifu wengi.
Bwana Yesu aliwaonya mitume wake mapema akawaambia..

Yohana16 :1 ‘Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa.
2 Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. 
Lakini hilo halitadumu siku zote, wakati wao umeshawekwa tayari, wote watakuja kuangamizwa katika ile siku ya Bwana,kwa yale mapigo makuu ya mwisho yatakayoachiliwa juu ya dunia nzima.(Ufunuo 16) watapewa kwanza wainywe damu ya watakatifu waliyoimwaga tangu Habili mpaka mtakatifu wa mwisho atakayeuliwa na wao, na baadaye watauliwa na kunyookea katika lile ziwa la moto.
Na ndio maana injili tuliyonayo sasa, si tu ya kuwaambia watu watoke dhambini, bali pia ni ya kuwahubiriwa watu kutoka katika DINI ZA UONGO. Watu wasije wakafa kwa kukosa kuzijua hila za shetani.
Mwisho kabisa, sauti ya Mungu kwetu ni hii:

Ufunuo 18: 4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU, MSISHIRIKI DHAMBI ZAKE, WALA MSIPOKEE MAPIGO YAKE.15 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake’’.

Hivyo kama wewe ni mtu wa Mungu, na sio wana wa majoka yaliyohusika kuua watu wa Mungu wasio na hatia watakatifu zaidi ya milioni 68, na bado wanaendelea sasa kwa siri, na watazidi sana katika kile kipindi cha dhiki kuu,..leo hii unaisikia sauti yake ikisema na wewe na kukumwambia mwanangu TOKA HUKO!!!

Usifanye moyo wako mgumu. Ondoka! Kwa furaha zote, uipishe ghadhabu ya Mungu.
Ukiulizwa wewe ni nani, sema mimi ni Mkristo hiyo inatosha..kwasababu ndio watakatifu wa kwanza, maBABA zetu wa imani mitume na manabii walivyoitwa, na hakukuwahi kuonekana dosari yoyote ya mauaji, au ya fitina ndani yao…Hao ndio mababa wetu. Tuwafuate wao.. BIBLIA TAKATIFU NENO LA MUNGU. Haleluya!!

Lakini Hawa mababa wengine hatujui watokako, asili yao ni upande mwingine wa adui…ni maadui wa msalaba, katika mavazi ya kondoo.
Ubarikiwe.

3 comments: