"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Wednesday, January 4, 2017

MASWALI YALIYOULIZWA NA MAJIBU YAKE: SEHEMU YA 9

SWALI 1: Ahsante ndugu napenda kujua sasa kama ngurumo saba ni watu hao saba watakaotoa ujumbe kila mtu tofauti tofauti kwa wakati mmoja(ufunuo 10) na bibi arusi ametawanyika kila kona mwingine vijijini ambako hakuna tv wala taarifa yoyote kusikika je yeye atapataje ujumbe huo ili kuamshwa?
JiBU:ufunuo sura  ya 10

1 Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto.
2 Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa kuume juu ya bahari, nao wa kushoto juu ya nchi.
3 Naye akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia, zile ngurumo saba zikatoa sauti zao.
4 Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie muhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike.
5 Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni,
6 akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya;
7 isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.
8 Na sauti ile niliyoisikia kutoka mbinguni ilinena nami tena, ikisema, Enenda, ukakitwae kile kitabu kilichofunguliwa katika mkono wa yule malaika, aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi.
9 Nikamwendea malaika yule nikamwambia kwamba anipe kile kitabu kidogo. Akaniambia, Kitwae, ukile, nacho kitakutia uchungu tumboni mwako, bali katika kinywa chako kitakuwa kitamu kama asali.
10 Nikakitwaa kile kitabu kidogo katika mkono wa malaika yule, nikakila; nacho kikawa kitamu kama asali kinywani mwangu, na nilipokwisha kukila tumbo langu likatiwa uchungu.
11 Wakaniambia, Imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi.
Baada ya ngurumo 7 kutoa sauti zao ambao ni watu 7, Mungu atakaowanyanyua wakati wa mwisho kuzungumza siri zilizopo katika kile kitabu kidogo kilichobeba siri za ukombozi wa mwanadamu ambazo katika hizo bibi arusi atapata imani ya kwenda kwenye unyakuo.
Lakini tunaona pia hapo kwenye mstari wa 8 Yohana alipewa kile kitabu akile, hapa Yohana anawakilisha bibi arusi wa kristo, na alipokila kile kitabu ambacho kilikuwa kitamu mdomoni mwake bali kichungu tumboni mwake, maana yake ni  kwamba ule ufunuo atakaoupata kutoka katika kile kitabu ambacho kitahubiriwa na zile ngurumo 7 utakuwa ni mzuri kuusikia lakini utakuwa ni mgumu kuupokea na kuuhubiri. kwahiyo kama tunavyoona kwenye mstari wa 10 yohana(bibi arusi) alivyoambiwa imempasa atoe tena unabii juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi, hii inamaana bibi arusi baada ya kuupokea ujumbe wa zile ngurumo 7, Roho kuu ya uvivuo itawajilia na ndio watakaopeleka injili duniani kote kwa mara nyingine tena, kwa udhihirisho mkuu wa Roho Mtakatifu kwa namna ambayo haijawahi kutokea kabla ili kuwa ushuhuda kwa mataifa yote, hapo ndipo ule mwisho utakapokuja(kama mathayo 24:14, inavyoelezea).
Kwahiyo ni dhahiri kuwa kuna uamsho mkuu unakuja mbeleni utakaopita dunia yote.
Kwahiyo ndugu, bibi arusi atasikia hizi jumbe popote alipo hiyo sio kazi kubwa kwa Mungu kuwaleta pamoja watu wake, palipo na mzoga ndipo watakapokusanyika tai. tabia ya tai sio kubaki sehemu moja wanatabia ya kuzunguka zunguka na macho yao yanaona kila mahali, vitu vyote vinavyofaa na visivyofaa, kwahiyo kama tai na sio kuku kwa msaada wa Roho Mtakatifu ukweli utawafikia popote walipo. Kwahiyo na sisi pia tuwe macho kwa maana hiyo saa ipo karibu. ubarikiwe sana.

SWALI 1.b:
ubarikiwe ndugu kwa ufafanuzi wa jambo hilo nitazidi kujifunza hapo naamini Mungu atanisaidi kulipata vizuri lakini kwa sehemu naamini ni kweli kuwa kutakuwa na uamsho wa bibi arusi maana ni kweli Yohana alipokila kile kitabu na hii ni sawa na lile gombo la chuo! Nalo lilikuwa chungu tumboni na tamu mdomoni. Na Yohana anaambiwa imempasa kutoa unabii juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi hapa ni kweli kabisa naliona hili kuwa ni mtembeo wa uamsho. Lakini shaka langu kidogo liko hapo kuwa je ni lazima wawe watu 7? Mungu hawezi kufunua siri au ufunuo huo ndani ya mioyo ya bibi arusi yeye mwenyewe kama vile alivyofanya kwa Yesu katika Yohana 12? Lakini katika swali nililouliza nimeona kweli bibi arusi anaweza kusikia kwa njia yeyote ile maana huyo ndiye Mungu atakayekuwa amemkusudia kwa maana hata nabii wakati anauleta ujumbe huu haujaandikwa popote lakini kuna watu kijijini kule kabisa  wanao wanauamini lakini pengine walioko mjini wengine hata wasiujue ambao tungetegemea kuwa ndo wangekuwa wameupata!.

JIBU: Mungu akubariki ndugu ni kweli unachosema inawezekana kabisa Mungu kuwafunulia watu wake siri hizo pasipo hata hao watu 7, lakini ni njia Mungu aliyoikusudia hizo ngurumo saba zitoe sauti zao kwanza kisha ndipo kuje uamsho wa bibi arusi duniani kote, mfano mzuri tunaona Bwana Yesu kristo jinsi alivyowachagua kwanza mitume wake 12, kupeleka injili kwa watu wa mataifa na israeli, lakini tunafahamu kuwa baadaye wakristo waliposikia injili ya mitume, ndipo ukatokea uamsho mkubwa, wale wakristo wakaanza kupeleka injili duniani kote. kwahiyo wale mitume 12 Mungu aliwateua kuwa kama waanzilishi wa imani. Naona ndivyo itakavyokuwa hata kwa ngurumo saba zitakapotoa sauti zao.

 SWALI 1.c: Lakini ndugu palipo na mzoga ndipo wakusanyikapo tai. Hii inamaana gani? kwa maana nimekuwa nikijiuliza kuwa tai hali mzoga nasikia anakula fresh. Sasa kwanini akusanyike katika mzoga na yeye si chakula chake? Hebu nipe ufahamu hapo ndugu na Mungu akubariki.

JIBU: kuhusu Tai, sio kila mfano wa tai unamuhusu yule tai asiyekula mizoga ambaye anawakilisha bibi-arusi, hapa tunapaswa tuelewe content ya huo mstari ulikuwa unamaana gani. Dhumuni kubwa la huo mstari sio kwamba sisi bibi arusi wa Kristo tunakula mizoga bali inaelezea tukio fulani litakalo sababisha au kumvutia bibi arusi kukusanyika pamoja na ndio maana pale alitumia mfano wa tai(vulture) na sio tai(eagle). tunajua eagle hali mizoga bali vulture, kwahiyo ili mfano ueleweke Yesu alitumia mfano wa vulture na mzoga. kwamfano unaweza ukaenda porini mahali ambapo huwezi tarajia kuona nzi, lakini ukitupa tu kitu kilichooza baada ya muda mfupi utaona inzi wengi wamekusanyika, utajiuliza ni wapi wametokea nzi hawa wote. Vivyo hivyo Yesu Kristo alitumia ule mfano kufundisha jinsi watu wake watakavyokuja kukusanyika katika kipindi cha mwisho baada ya hizo jumbe za kipekee kushushwa(ngurumo saba ufu. 10) na ndio maana tunasema bibi arusi atajua mahali mzoga (kweli ya Mungu) ulipo mahali popote hajalishi yuko wapi, Roho Mtakatifu atampeleka mahali hicho chakula kilipo. Mungu akubariki. soma y

Yohana 16:13" Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.
15 Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari."


SWALI 2:
Shalom ndugu Kitabu cha ESTA kina uhusiano gani na NYAKUO?

JIBU: Habari ya Esta tunaweza tukaichambua kama ifuatavyo;
  • Mfalme Ahausiero anayezungumziwa pale ni mfano wa BWANA YESU KRISTO
  • Vashti ambaye ni malkia aliyeonyesha otomvu wa nidhamu ni  mfano wa ISRAELI
  • wanawali wengine wote waliotoka kwenda kujionyesha mbele ya mfalme wale ni mfano wa MAKANISA YOTE ULIMWENGUNI TULIYONAYO sasa  kwamfano katoliki, wasabato, walutheri, waanglikana, wamethodisti, branhamite, wapentekoste n.k
  • Ester pale anawakilisha  Bibi arusi wa Kristo safi  (bride of christ).
  • na Hegai msimamizi wa nyumba ya mfalme anawakilisha "Mjumbe wa wakati wa saa"


kwahiyo kama tunavyoielewa habari vashti alivyomvunjia heshima mfalme pale alipoitwa ajionyeshe mbele ya mfalme karamu ilipoandaliwa, ni picha halisi kabisa ya israeli walivyomkataa Yesu Kristo kama mfalme wao, na kumwaibisha kwa kumpeleka msalabani, na jinsi tunavyoona sehemu ya vashti kama malkia iliondolewa na kupewa mwingine, hiyo inaonyesha ile nafasi ya waisraeli kuwa kama malkia wa kristo ilihamishwa na kupelekwa kwa mataifa, na kama tunavyoona mfalme baada ya kumfukuza Vashti alianza kutafuta malkia wake mwingine katika mataifa yote duniani, vivyo hivyo wayahudi baada ya kumkataa Yesu, Yesu alianza kutafuta malkia wake katika mataifa yote duniani.  Na kama tunavyoona wale mabikira walivyoenda kujihudhurisha mbele ya mfalme ni mmoja tu aliyekubaliwa na mfalme ambaye ni Esta vivyo hivyo katika kanisa la mwisho ni bibi arusi wa kristo mmoja tu atakayekuwa malkia, na atakayekubaliwa na Yesu Kristo ingawa wengi wanajihudhurisha mbele yake.  
lakini swali ni je! kwanini Esta akubalike mbele ya mfalme kuliko wanawali wengine wote?? je yeye alikuwa ni mzuri sana kushinda wengine?   
siri ni moja nayo ilikuwa ipo kwa Hagai mwangalizi wa nyumba ya mfalme. Huyu Hagai alikuwa akikaa katika nyumba ya mfalme kwa muda mrefu, na ndiye aliyekuwa muhudumu wa Vashti, alitambua vigezo vyote mfalme alivyovutiwa  kwa malkia, alikuwa anafahamu kwa undani vigezo vilivyomfanya hata mfalme ampendee Vashti, hivyo basi wakati wale wanawali wengine wapo buzy kwenda kwa urembo wao mbele za mfalme ili wachaguliwe kama malkia, Esta yeye alijikabidhisha kwa Hagai mwangalizi wa nyumba ya mfalme na alikuwa anafanya chochote ambacho anaambiwa, Hivyo Hagai alimpa Esta siri za kwenda kujihudhurisha mbele ya mfalme ili achaguliwe,jambo ambalo wale wengine wote hawakuweza kulijua. na mfalme alipomwona alivutiwa na Esta kuliko wanawali wengine na kuteuliwa kuwa malkia sehemu ya Vashti.
swali ni je! leo hii Hagai wetu ni nani? atakayetufundisha sisi tukubalike mbele ya mfalme ambaye ni YESU KRISTO? 
Mjumbe wa kanisa la saba,(willam branham) Mungu alimtuma kwa kizazi chetu kuleta ujumbe wa kuturujesha katika vigezo vya kukubaliwa na Bwana(yaani NENO ). bIbi arusi wa Kristo(Esta) atafuata hivyo vigezo, atashikilia neno tu na sio kingine, wakati anaenda kujihudhurisha mbele za BWANA wakati wengine wanaenda kwa mitazamo yao na desturi zao, na uzuri wao, na mifumo yao wakidhani watakubaliwa mbele za Bwana Esta yeye ataenda na Neno. na mfano wa hawa wanawali wengine ambao hawakukubalika mbele za mfalme, ni Madhehebu tuliyonayo sasa, kama katoliki, lutherani, anglican, branhamites, pentecoste,methodist, mashahidi wa Yehova,baptist, presibyterian n.k. 
Kwahiyo Kristo hawezi kuja kulichukua kanisa lililovunjika vunjika hivi, kila mmoja anajiona bora kuliko mwenzake, hawajui ni kitu gani mfalme anavutiwa nacho, wanadhani kuwa na majengo mazuri, kuwa na watu wengi, kuwa na miradi, kuwa maarufu, kwamba ndio Mungu anapendezwa nao, wamelitupa NENO la Mungu mbali, lakini Bwana anamwandaa Esta wake ambaye atasema 'NDIO' kwa maneno yote ya Mungu bila kujali jambo lolote. Aleluya!!

No comments:

Post a Comment