"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Wednesday, January 11, 2017

TOKENI KWAKE ENYI WATU WANGU-7

Ufunuo 18:
1 Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.
2 Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;
3 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.
4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.
Biblia imetuonya katika hichi kipindi cha mwisho tujitenge na ile dini ya Babeli, Mungu ametuita kuwa bikira safi, na ni bikira safi tu asiye na mawaa ndiye atakayeingia katika karamu ya mwanakondoo, Wakristo wengi sasa tunasema sisi ni wakristo lakini sio ukristo halisi wa kwenye biblia ambao ulihubiriwa na mitume, lakini ukristo uliopo sasa ni madhehebu, embu tujiulize je! Kristo amegawanyika, au Bwana Yesu akirudi leo atachukua dhehebu gani aliache dhehebu gani? kwahiyo ni wazi kabisa kuwa udhehebu sio ukristo, maana palipo na madhehebu pana mapungufu, lakini ukristo hauna mapungufu. Kwahiyo unapoacha kuwa mkristo sawa sawa na maandiko na kujifungia na kufuata miiko au taratibu za dhehebu fulani, hata kama haviendani na maandiko, na kuweka neno la Mungu kando kama taa yako ya kukuongoza hapa duniani, huko ndiko kufanya uasherati wa kiroho kwa maana ingekupasa kulifanya lililo sahihi lakini ukageukia mafundisho mengine, Hivyo basi madhehebu yote Mungu ameyahukumu, na ndiyo yaliyoibeba ile chapa ya mnyama ndani yake. Na ujumbe wa sasa kwa wakristo wote ni huu. "Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake",  
Unapousikia ujumbe huu, ufanye hima utoke, na sio utoke kwa miguu au ubadilishe kanisa, hapana bali utoke kwa kuutafuta ukweli na kuoana na neno la Mungu, ujazwe Roho wa Mungu. na Roho ndiye atakayekuongoza katika kuijua kweli yote, sio dhehebu wala shirika lolote la dini wala kanisa, tafuta uhusiano wako binafsi na Yesu Kristo na ndipo utakapokuwa bikira safi.  
Mungu akubariki!

No comments:

Post a Comment