SWALI: Watumishi naomba kuuliza..ni nani anatawala dunia kati ya Mungu na shetani? Na kama ni Mungu anayetawala kwa nini kuna matukio ya kutisha kama ajali mbaya za magari,ndege,mafuriko kama ya Japan kama Mungu ndiye anayetawala kwanini hayazuii anaacha yanaua watu??? Na ukisoma mathayo 4:1 na kuendelea unasoma shetani anamwambia Yesu dunia ni Mali yake, na Kuna tofauti gani kati ya dunia na ulimwengu nisaidie?
JIBU: Dunia yote ni ya Mungu ukisoma;
zaburi 24: 1-2 "1 Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake.Na pia Bwana Yesu Kristo baada ya kufufuka kwake aliwaambia wanafunzi wake
2 Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. "
mathayo 28:18"Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. "Kwahiyo kwa maandiko hayo tunaona kabisa dunia yote inamilikiwa na Mungu na wala sio shetani, lakini "dunia sio ulimwengu". Huu ulimwengu ndio mali ya shetani na ndio yeye anayeumiliki na kitakachokuja kuteketezwa sio dunia bali ni ulimwengu huu mbovu wa shetani ambao ni milki yake..
Tofauti kati ya dunia na ulimwengu ni hii;
- Dunia ni vitu vyote vya kijeografia unavyoviona vya asili kama mabara, bahari, miti, milima, hewa, ardhi, mito,mabonde, visiwa, n.k.
- Na Ulimwengu ni ustaarabu uliobuniwa na aidha Mungu au shetani ili kuifanya dunia iwe ni mahali pa kuishi. mfano. elimu, burudani, miziki, utawala, uchumi, mahakama,Milki, fahari, uchukuzi, n.k. Na ndio maana kwenye mathayo 4 shetani alimwambia Bwana Yesu nitakupa ulimwengu wote na fahari yake ukianguka kunisujudia.
Na sababu ya Mungu kuruhusu mambo mabaya kutokea kama ajali, vimbunga, mafuriko ni kwasababu ya mambo maovu ya huu ulimwengu yaliyopo kama umwagaji damu, rushwa, uasherati, ulevi, uaribifu wa mazingira, ushoga, vita, n.k. mambo kama haya huaribu dunia husababisha gadhabu ya Mungu kumwaga juu ya nchi.
No comments:
Post a Comment