"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Friday, December 28, 2018

MASWALI NA MAJIBU: SEHEMU YA 48


SWALI 1: HOSEA 3 Kwa nini MUNGU Anampa Nabii Hosea maagizo ya Kumuoa mwanamke kahaba?

 JIBU: Mungu alimpa maagizo nabii Hosea kuoa mke aliye kahaba, sio kwasababu Mungu, anahalalisha usherati, hapana! Kusudi la Mungu kufanya vile ni kutaka kuwaonyesha wana wa Israeli ni jinsi gani wao wanavyofanya uasherati katika roho zao mbele zake kwa kuyaacha maagizo  yake..

Kwahiyo nabii Hosea alipooa mke wa uzinzi, ilikuwa kama ishara ya Bwana kutaka kuwaonyesha wana wa Israeli mambo wanayoyafanya mbele zake…Sasa Bwana alitaka endapo watu watakapomwuliza Hosea kwanini ameoa mke ambaye ni mzinzi…ndipo Hosea awajibu, kama mimi ninavyoudhiwa na huyu mwanamke mzinzi ndivyo na ninyi (wana wa Israeli) mnavyomuudhi Bwana kwa kufanya uzinzi mbele zake kwa kulihalifu agano lake na kuabudu miungu migeni, ukisoma habari ile yote kwa urefu utaona jambo hilo.


Sio mara ya kwanza Bwana kutoa ishara kupitia maisha ya watu, ukisoma biblia mahali pengine utaona Nabii ezekieli Bwana anamwagiza ale kinyesi, mahali pengine akate nywele zake kwa upanga azigawanye sehemu tatu….sehemu nyingine anaambiwa ahame nyumba yake kwa kutoboa ukuta, huku amejifunika macho kumwonyesha Mfalme wa Yuda Sedekia kwamba wakati majeshi ya wakaldayo yatakapouzingira mji kwa miaka miwili, yeye atatoroka kwa njia ya kutoboa ukuta wa mji, na hatimaye watamkamata na kumtoboa macho yake sawasawa na nabii Ezekieli alivyoonyesha…


Ezekieli 12:1-15

"1 Neno la Bwana likanijia tena, kusema,

2 Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi.

3 Basi, mwanadamu, funga tayari vyombo kwa uhamisho, ukahame wakati wa mchana mbele ya macho yao; nawe utahama toka mahali pako hapa mpaka mahali pengine mbele ya macho yao; labda watafahamu, wajapokuwa ni nyumba iliyoasi.

4 Nawe utatoa vyombo vyako, wakati wa mchana, mbele ya macho yao, kana kwamba ni vyombo vya kuhamishwa; nawe mwenyewe utatoka, wakati wa jioni, mbele ya macho yao, kama watu watokavyo katika kuhamishwa.

5 Toboa mahali ukutani mbele ya macho yao, ukachukue vitu kwa kuvipitisha pale.

6 Mbele ya macho yao utajitwika begani pako, na kuvichukua nje gizani; utafunika uso wako, hata usiione nchi; kwa maana nimekuweka uwe ishara kwa nyumba ya Israeli.

7 Nikafanya vile vile kama nilivyoamriwa; nalitoa vyombo vyangu wakati wa mchana kana kwamba ni vyombo vya kuhamishwa, na wakati wa jioni nikautoboa ukuta kwa mkono wangu; nikavitoa gizani, nikavichukua begani, mbele ya macho yao.

8 Asubuhi neno la Bwana likanijia, kusema,

9 Mwanadamu, nyumba ya Israeli, je! Nyumba ile iliyoasi, hawakukuambia, Unafanya nini wewe?

10 Waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Ufunuo huu wamhusu mkuu wa Yerusalemu, na nyumba yote ya Israeli walio kati yao.

11 Sema, Mimi ni ishara kwenu; kama mimi nilivyotenda, wao nao watatendwa vile vile; watahamishwa, watakwenda kufungwa.

12 Naye mkuu aliye kati yao atachukua begani katika giza; naye atatoka kwenda zake; watatoboa mahali ukutani, wapate kuvichukua vyombo vyao nje; atafunika uso wake, kwa sababu hataiona nchi kwa macho yake.

13 Tena wavu wangu nitautandika juu yake, naye atanaswa kwa mtego wangu; nami nitampeleka Babeli, mpaka nchi ya Wakaldayo; lakini hataiona, angawa atakufa huko.

14 Nami nitawatawanya kwa pepo zote wote wamzungukao ili wamsaidie, na vikosi vyake vyote; nami nitaufuta upanga nyuma yao.
15 Nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana; nitakapowatawanya kati ya mataifa, na kuwatupa-tupa katika nchi zote”
  *Ukizidi kusoma utaona mahali pengine Nabii mmoja Bwana alimwagiza amwambie mtu ampige mpaka atoke majeraha.

1 Wafalme 20: 35 “Basi, mtu mmoja wa wana wa manabii akamwambia mwenzake kwa neno la Bwana, Nipige, nakusihi. Akakataa yule kumpiga.

36 Akamwambia, Kwa sababu hukuisikiliza sauti ya Bwana, angalia, mara ukitoka kwangu simba atakuua. Na mara alipotoka kwake, simba alimwona, akamwua.
37 Ndipo akaona mtu mwingine, akasema, Nipige, nakusihi. Yule mtu akampiga, hata kumpiga na kumtia jeraha.”

Sasa mambo haya yote ni ishara ya Bwana kutaka kuzungumza na wana wa Israeli kwa kupitia maisha ya watu, kwahiyo hiyo ndio sababu ya Mungu kumwambia Nabii Hosea akaoe mke wa kikahaba..na pia kumbuka Hosea mwenyewe hakuwa mzinzi ni yule mwanamke aliyeambiwa amwoe ndiye aliyekuwa ni kahaba. Kwa jinsi hiyo hiyo mambo hayo yanavyochukiza mbele za watu ndivyo hivyo hivyo yanavyochukiza mbele za Mungu, pale watu wanapoasi maagano yake.


Ubarikiwe!SWALI 2: Milele tunafahamu ni kitu ambacho hakina mwisho.Swali ni kwamba Yuda1:6"Na Malaika wasiolinda enzi yao wenyewe,lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu,amewaweka katika VIFUNGO VYA MILELE CHINI YA GIZA kwa hukumu ya siku ile...

Swali hapo ndugu zangu hiyo LUGHA iliyotumika hapo"VIFUNGO VYA MILELE"hapo inamaana gani..Kwanini imesema vya "milele" badala ya kusema vya daima au vya Muda fulani?.JIBU: Nafikiri hili swali tulishalijibu kipindi fulani nyuma...Lugha yetu ya kiswahili ina mipaka, au tunaweza tukasema haijitoshelezi kwa baadhi ya tafsiri, kwahiyo inagharimu kutumia neno la ujumla kumeza tafsiri mbili au zaidi..kwamfano ukitaka kutafsiri neno la kingereza linalosema  “she came here yesterday” tafsiri yake ni  “alikuja hapa jana”…kadhalika ukitaka kutafsiri neno “he came here yesterday”..utaona ni kitu kile kile “alikuja hapa jana”…kwahiyo utaona kwamba lugha yetu katika kutafsiri inameza baadhi maneno, unakuta hatuna tafsiri ya neno kama “he” au “she” katika sentensi zetu na maneno mengine mengi ni ivyo hivyo.

Kadhalika  ukirudi katika biblia yetu ya kiswahili imetafsiriwa kutoka katika lugha ya kigiriki ambayo ndio iliyoandikia biblia..sasa kuna baadhi ya maneno hatuna tafsiri nayo katika lugha yetu..

Kwamfano tuchukue maneno la kingereza “everlasting” na “eternity”..Haya maneno mawili yanatafsiri zinazokaribia kufanana sana, lakini hayafanani...everlasting maana  yake “kwa muda mrefu sana” na “eternity” maana yake “milele isiyokuwa na mwisho”..Sasa katika biblia ya kigiriki tafsiri hizi za maneno haya mawili zimetofautishwa…lakini kwa katika tafsiri yetu hayajatofautishwa..mahali panapopaswa patumike kama “everlasting” pametumiwa “eternity” na mahali pa pa eternity pametumika ivyo hivyo eternity. Kwasababu lugha yetu haijitoshelezi.

Sasa wote waliomwamini Kristo hao Bwana kawaahidia uzima wa milele yaani “eternal life” na sio “everlasting life”..lakini wote ambao hawajampokea yeye biblia inasema watahukumiwa kwa moto wa milele..sasa huo umilele uliozungumziwa kwa wote ambao hawajampa Bwana maisha yao sio umilele wenye tafsiri ya “eternity” hapana bali ni wenye tafsiri “everlasting” yaani “moto wa muda mrefu”..lakini kwa kuwa lugha yetu neno “everlasting na eternity” ina tafsiri moja “milele” ndio maana unaona kote biblia inataja watakaohukumiwa watahukumiwa kwa moto wa milele lakini sio sahihi…Uzima wa milele upo kwa Yesu tu peke yake!! Hakuna  mtu au kiumbe chochote kitakachopata uzima wa milele nje ya Yesu Kristo..vingine vyote vitaadhibiwa kwa moto wa kudumu muda mrefu sana na hatimaye baada ya kipindi fulani kirefu sana vitapotea kabisa milele..kwasababu havina uzima wa milele..

Ubarikiwe!

SWALI 3: Waebrania1:5"Kwamaana(Bwana Yesu)alimwambia MALAIKA YUPI wakati wowote,NDIWE MWANANGU,..? Tunaona hapo Roho akituuliza ni Malaika yupi ambaye Mungu amemuita Mwanangu?.akasema kwa habari ya Malaika kwamba "Hao ni roho watumikao,wakitumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu[Hapo anapinga kuwaita Malaika wa mbinguni Wana wa Mungu.Waebrania1:14]".


Tukirudi agano la kale anasema"Ilikuwa,siku moja ambayo hao WANA WA MUNGU walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA[Ayubu1:6]:.. 

Ndugu zangu kama mlivyofundisha leo[Kwenye lile somo la HUDUMA YA MALAIKA WA MBINI] kwamba hao wana wa Mungu wanaotajwa hapo(Ayubu1:6)ni Malaika wa mbinguni".Nilikuwa silifahamu hilo ndugu zangu.Sasa nikawa na swali mbona katiki hicho kitabu cha Waebrania anapinga kuwaita hao malaika wa mbinguni WANA WA MUNGU Lakini Kama mlivyofundisha leo kwenye kitabu cha Ayubu anawaita Malaika wa mbinguni WANA WA MUNGU?.


JIBU: Ni kweli maandiko yanasema Malaika sio wana wa Mungu, lakini hiyo ilikuwa ni maana kwa ujumla..inategemea mahali neno hilo wana wa Mungu linapotumika..katika kitabu cha mwanzo wana wa Mungu waliozungumziwa pale ni wanadamu, lakini katika kitabu cha Ayubu ni malaika...
Kwahiyo Hiyo hilo neno wana wa Mungu..wakati mwingine linatumika kama neno la ujumla kuwakilisha familia ya Mungu..ambayo ni wanadamu na malaika. Ubarikiwe! Mfano mzuri ni neno Malaika lenyewe...mahali pengine katika maandiko malaika wanatumika kama wajumbe wa kiroho kutoka mbinguni...lakini ukirudi kwenye kitabu cha ufunuo sura ya 2 na ya 3 utaona malaika wanaozungumziwa pale wa yale makanisa saba ni wanadamu...kwahiyo wana wa Mungu na malaika ni majina yanaoingiliana na wanadamu na malaika.

 Ubarikiwe!

No comments:

Post a Comment