Baada ya Bwana Yesu kufufuka,
tunasoma habari ya vijana wawili waliokuwa wanaenda kijiji kimoja kilichopo mbali
kidogo na mji wa Yerusalemu, na walipokuwa njiani wakizungumza habari za kufufuka
kwa Bwana biblia inatuambia Bwana wenyewe aliungana nao pasipo hata wao kujua,
kwani macho yao yalifumbwa wasimtambue
lakini baadaye mwisho wa safari yao walikuja
kumtambua..tunasoma habari hiyo katika..
Luka 24.13 “Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili.
14 Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia.
15 IKAWA KATIKA KUZUNGUMZA NA KUULIZANA KWAO, YESU MWENYEWE ALIKARIBIA, AKAANDAMANA NAO.
16 Macho yao yakafumbwa wasimtambue.
17 Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao.
18 Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi?
19 Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote;
20 tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha.
21 Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo;
22 tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema,
23 wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai.
24 Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona.
25 Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!
26 Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake?
27 Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.
28 Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, NAYE ALIFANYA KAMA ANATAKA KUENDELEA MBELE.
29 Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao.
30 Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.
31 Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao.
32 Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko?”.
Wengi
tunatamani Kristo atutokee siku moja, na kuanza kutembea nasi, ndipo tuamini
Yupo na sisi, lakini hatujui kwamba Kristo yupo pamoja na sisi kila siku,
akitufundisha na kutufunulia maandiko…kama Neno lake linavyosema “walipo
wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”…Unaona hapo kwa wakati
huo Macho yetu ya mwilini yanakuwa yamefumbwa yasimwone lakini macho yetu ya
rohoni yanamwona.
Ndicho
kilichowatokea hawa watu wawili waliokuwa wanaenda Emau..Bwana alipojiunga
katikati yao Macho yao ya mwilini yalifumbwa wasimtambue lakini macho yao ya
rohoni yalikuwa yanamwona Bwana, alipokuwa anawafunulia maandiko kumhusu yeye.
Ni
kwanini Bwana alijiunga nao? Ni kwasababu “tayari walikuwa wameshakusanyika
wawili kwa jina lake, wakizungumza habari zake” ..hivyo Kristo lazima atimize
Neno lake “la kuwepo katikati yao”.
Sasa
maana ya kuwepo katikati yao sio kumwona sura yake hapana! Bali kumwona yeye
katika Neno lake. Ndio maana wale watu
wawili Bwana hakuwafumbua macho yao wamwone sura yake, bali alianza kwanza
kuwafunulia maandiko wamwone yeye katika Neno lake.
Kwahiyo
unaweza kuona Bwana havutiwi sana, na sisi kumwona yeye uso wake, bali
anavutiwa sana na sisi kumwona yeye katika Neno lake. Ndio maana leo hatokei
wengi, kwasababu anataka tumjue katika Neno lake, zaidi ya uso wake.
Ukiendelea
kusoma habari za hawa vijana wawili, utagundua hata baada ya Bwana kumaliza
kuwafunulia maandiko, hakutaka kuwafumbua macho ya mwili wamwone, badala yake
utaona alitaka kuondoka kuwaacha katika hali ile ile ya kutomtambua, alitaka
kuendelea mbele na safari yake, Ni kwanini alifanya vile? Ni kwasababu lengo
lake halikuwa kuwaonyesha uso wake, bali lengo lake lilikuwa wamwelewe katika
maandiko..Na baada ya kutimiza kusudi lake la kuwafunulia maandiko kazi ilikuwa
imeshakwisha, alitaka kutengana nao... Lakini walipomshawishi sana ndipo akaamu
kwenda kula nao, na huko ndio
akawafumbua macho yao ya mwilini wamwone.
“28 Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa
wakienda, NAYE ALIFANYA KAMA ANATAKA KUENDELEA MBELE.
29 Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi,
kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao”.
Na ndio maana tunakuja kusoma pia Bwana
alimkemea Tomaso kwa kutokumwamini…yeye alitaka auone uso wa Bwana na majeraha
yake ndipo aamini, lakini Bwana hakutaka amwamini kwa njia hiyo..alitaka Tomaso
amwamini kwa njia ya maandiko?..alitaka Tomaso amwamini kwa ufunuo wa maandiko,
sio kwa kumwona uso..alitaka Tomaso amtambue yeye kwa kuyajua yaliyotabiriwa
kumhusu yeye kuanzia kwa Musa, zaburi na kwa manabii wote, na hayo mengine yawe
baadaye sana kama yanaumuhimu.
Ndugu sura ya Yesu haiwezi kutufanya tumwamini
yeye hata kidogo, kitakachotufanya tumwamini Bwana Yesu ni ufunuo katika Neno
lake, ni kumtambua kupitia Neno lake, kumwona ametabiriwa wapi katika maandiko,
na nafasi yake ni ipi katika Roho sasa.
Wanafunzi hata baada ya kumwona Bwana YESU uso
wake,akiwa amefufuka hawakumwamini, walimtilia mashaka, walidhani wanaona
mizimu..Na hata kama Bwana angewatokea mara 100 kama asingewafunulia akili zao
wayaelewe maandiko wasingemwamini…wangeendelea kumtilia mashaka tu!..Tunaona
mtu kama Yuda yeye sio kutokewa tu
dakika chache halafu basi, hapana bali yeye aliishi, alikula, alilala na Yesu
lakini mwisho wa siku akaja kumsaliti.
Luka 24.36 “Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu.
37 Wakashituka, wakaogopa sana, wakidhani ya kwamba wanaona roho.
38 Akawaambia, Mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu?
39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.
40 Na baada ya kusema hayo aliwaonyesha mikono yake na miguu yake.
41 Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula cho chote hapa?
42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa.
43 Akakitwaa, akala mbele yao.
44 Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi.
45 NDIPO AKAWAFUNULIA AKILI ZAO WAPATE KUELEWA NA MAANDIKO.
46 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;
47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu”.
Je!
na wewe leo amefunua akili zako, ili upate kuyaelewa maandiko??..ukiona huna
hamu ndani yako ya kuyasoma maandiko, na hakuna msukumo wowote ndani yako wa
kupenda kusoma Neno, mwombe Bwana leo hii akupe Neema…akupe hiyo nguvu, maana
hawezi kukufunulia macho yako ya rohoni uyaelewe maandiko kama maandiko
huyasomi… kuna hatari kubwa sana ya kukosa kulijua Neno la Mungu.. Kumbuka
Kristo hakufungui macho uuone uso wake yeye, wala halitamani hilo…ingekuwa anataka
tuuone uso wake, angeruhusu wakati ule picha yake ichorwe na iifadhiwe kwa
vizazi vyetu hivi, kama neno lake limeweza kuhifadhiwa kwa vizazi vyote hivyo
si zaidi picha? Ni kitu kidogo sana kuifanya picha yake ihifadhiwe kwa vizazi
vyote lakini hakutaka… au angekuja kipindi hichi cha teknolojia ambapo kila mtu
angeweza kumpiga picha na kuweka katika chumba chake cha ndani…Lakini hiyo sio
njia anayoitumia ili sisi tumwamini yeye…yeye anataka tumwamini yeye, na
tumjue, na tumfahamu sana kwa ufunuo wa Neno lake, biblia takatifu. Tukimtafuta
katika nyuso tutamkosa hayupo huko…alimwambia Tomaso wana heri wale wasioona
wakasadiki.
Je!
na wewe ndugu unamtafuta Bwana leo kwa njia ipi? Kwa njia ya uso au
maandiko?...Je Bwana amefunua akili zako uweze kumwona? Unasema unampenda Yesu
wa kwenye picha au Yesu wa kwenye maandiko?..Na kama ni wa kwenye maandiko je!
unayapenda maagizo yake yote aliyoyatoa?. Je! unajumuika na wengine wenye imani
moja na wewe kwa maana alisema “wakusanyikapo wawili watatu kwa jina lake atakuwepo
katikati yao”. Ni lazima tukusanyike kuanzia wawili na kuendelea ili Kristo,
ajumuike pamoja nasi kutufunulia maandiko. Ni muhimu sana kuhudhuria bible
study, au kukusanyika na mwenzetu kujifunza biblia kila iitwapo leo maadamu
siku ile inakaribia, ndipo tutakapomwona Yesu.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali
“share” ujumbe huu kwa wengine, Bwana akubariki.
No comments:
Post a Comment