Mbarikiwe sana ndugu zangu, Ndugu zangu naomba nisaidieni kupata tafsiri ya hii hii njozi maana imenitatiza sana:
Niliota kwamba BWANA YESU KRISTO amekuja duniani .lakini alipokuja aliwakuta watu baadhi wakiendeleea na shughuli zao (hawakujua kuwa amekuja) .na alipo fika alichukua watu baadhi akatoka nao kidogo nje ya kijiji kile (lakini kuna mtu mwingine alisema kwamba kuna kitu amesahau sehemu basi akaamua kukirudia hicho kitu ;huku wale wengine ambao BWANA YESU kawatoa nje ya kijiji wakiambatana nae)_..
Sasa tulipofika mwisho wa kijiji kile (pembezoni mwa kijiji ) BWANA YESU akasema anaanza kubagua Kondoo na mbuzi kwenye lile kundi alilotoka nalo kwenye kile kijiji .. .tulipokuwa katika kujiandaa ghafla nikaona Kondoo na mbuzi mbele yetu ..basi watu wakaanza kwenda kwenye Kondoo na wengine kwenye mbuzi..
Bwana alipomaliza kuwabagua .akaenda tena kwenye ndicho kilicho nishangaza AKAANZA TENA KUWABAGUA HAO KONDOO TENA. alikuwa ananyosha kidole mkono wa kulia wanakuja kwake.. Lakini walikuwa kama wanataka kugombaniana kwenda kwa Bwana. Kati ya lile kundi walitoka watu wachache sana wa kwenda na Bwana. Sasa baada ya kuwachagua Bwana akaenda kama kwenye kitu cha usafiri hivi.(sikukifahamu ) na alipofika akaingia kwanza na sisi tukafuata nyuma lakini kabla ya kuanza kuingia akafika yule aliye omba ruhusa kule mwanzo afuate kitu sehemu akasema nae anasitahili awe na BWANA lakini Bwana hakumkubalia .. Yule ndugu alilia sana akisema nae anastahili kuingia kwenye ule usafiri.
Na nilipokuwa nawaangalia ndugu niliokuwa nao sikumwona hata mmoja ninaye fahamiana nae.( hata mama yangu sikumwona hata baba ,wadogo zangu,hata ndugu na dada zikumwona hata mmoja) .ndio nikaaanza kusikitika nikitaka kulia ghafla ikaja sauti ikiniambia kwamba (nilikuwa kama nafikiria ikisema HAKITAINGIA KILICHO KINYONGE .na tena ikasema kwamba WALIO CHAGULIWA KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU.).
Ndipo nikasikia Bwana akisema akimwita ndugu fulani..nilisika akisema PETRO KUNA CHAKULA .NIKAMWONA BWANA KAMA ANAANDAA CHAKULA HIVI. (Lakini cha kushangaza haya yote yalikuwa yakifanyika chini duniani) Baada ya hapo nikaona Mwanga mkali mbinguni. Hapohapo nikaamka . Nini maana yake ya hii njozi MUNGU wa mbinguni awafunulie maana yake. Shalom.
Ni wazi kuwa Bwana amekuonyesha maono ya siku za mwisho..Na
ndoto hiyo tutaichapisha ili na wengine pia wanufaike kwasababu ujumbe huo
haukuhusu wewe mwenyewe bali pia unalihusu
kanisa la Kristo kwa ujumla, ambao ni sisi sote humo humo kwa ujumla.
Kwanza kuwa upande wako unapaswa uamini kuwa bibi-arusi wa Kristo ni tofauti na
Kanisa la Kristo kwa ujumla, mke ni tofauti na suria japo wote wanaweza kuwa ni milki ya Bwana arusi .Maana yake ni
kuwa wanaoitwa wakristo ni wengi lakini bibi-arusi wa Kristo ni wachache sana,
na ndio hao peke yao watakaokwenda kwenye unyakuo, na kutokana na uchache wao
dunia haitajua kitu kitakachokuwa kinaendelea.,
Tofauti na watu
wengi wanavyodhani kuwa unyakuo ukifika
duniani kote kutakotekea machafuko ya kila namna, kila mtu atajua, ajali zitatokea
mabarabarani, mamilioni ya watu watapotea, kana kwamba njia ya mbinguni ni njia
nyepesi kuiingia kama shetani anavyowadanganya watu, biblia inasema kule
hakitaingia kilicho kinyonge, na kama ingekuwa wengi Bwana asingesema Kama
ilivyokuwa katika siku za Nuhu, Embu kaa chini ufikirie siku za Nuhu walipona
watu wangapi kama sio watu nane(8) tu kati ya mabilioni ya watu waliokuwa
ulimwenguni?, Bwana asingesema tena kuja kwake kutafanana na kama
zilivyokuwa siku za Lutu, siku zile
walipona watu watatu (3) tu kati ya malaki ya watu waliokuwa katika miji
ile…Ukisoma tena mahali pengine alisema “mlango ni mwembamba, na njia imesonga
iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.(Mathayo 7:14)”..Yote hayo
yanathibitisha kuwa mbinguni sio kurahisi kama watu wanavyokufikiri au
wanavyofundishwa.. Unyakuo hautakuwa kwa mtu yeyote ambayo hajaonyesha nia ya
kuuingia, sio kusema tu nimeokoka basi! Na kuendelea kuishi mtu anavyojisikia.
Na ndio maana hapo kwenye ndoto umeona kumbe hata katikati
ya kondoo bado kulikuwa na mchujo..Hiyo inalingana na maandiko kabisa kama
tukitazama mfano wa wale wanawali 10, (Katika Mathayo 25) ambao wote walikuwa
ni wanawali (mabikira) safi, wote walikuwa wanamsubiria Bwana wao, isipokuwa
katikati yao wengine walikuwa wenye busara na wengine wapumbavu. Wale wenye
busara walichukua taa zao pamoja na mafuta ya ziada, lakini wale wapumbavu
hawakubeba mafuta ya ziada katika vyombo vyao, na wakati ambao Bwana wao sasa
anakuja ili awachukue taa zao zikawa zinaanza kuzima , Hivyo wale wapumbavu
wakawaomba wenzao wawapunguzie kidogo, lakini wale wakasema hapana tukiwapa
hayawezi kututosha sisi pamoja na nyie ni heri mshike njia mkanunue ya kwenu,
na walipokwenda kununua, wakati wanarudi wakakuta tayari mlango
umeshafungwa..Bwana akawaambia Amin, nawaambia, siwajui ninyi.
Unaona? Siku hizi ni siku za mwisho, na inasikitisha kuwa
idadi kubwa ya watu wanaojiita ni wakristo sio wakristo kweli kweli, wanaitwa
hivyo kwasababu tu wamezaliwa katika familia za kikristo, lakini ukiangalia
mienendo yao, tabia zao, uvaaji wao, mazungumzo yao, yapo mbali kabisa na
Ukristo, yaani ni wakristo-jina.
sasa hao ni ndio wale mbuzi uliowaona wakitengwa mbali na
wale kondoo…Kadhalika wapo ambao kweli walianza vizuri na Bwana walisimama
imara lakini ilifika wakati wakaanza kupoa mguu mmoja ukawa nje, mwingine ndani, mwanzoni macho yao
yalikuwa yakielekea mbinguni, wamejitenga mbali na dhambi, wamethibitika katika
imani lakini ikafikia wakati wakaanza kupoa mfano wa wale wanawali wapumbavu
ambao hawakuwa na mafuta ya ziada katika taa zao. Na mafuta ya ziada ni UHAI WA
ROHO WA MUNGU NDANI YA MTU. Sasa wakaanza kumzimisha Roho wa Mungu ndani yao,
huko nyuma walianza vizuri lakini kidogo kidogo, wakaanza kupoa, mambo ya
ulimwengu huu yakaanza kuwasonga, lakini ukiwatazama huwezi kujua kuwa
wanamizigo ya kando inayowavuta, ibadani wanahudhuria, watavaa mavazi ya
kujisitiri, hata katika maombi utawakuta, wanafanana kabisa na wale wakristo
waaminifu waliosimama imara mbele za Mungu kwa uaminifu wote,isipokuwa wao ni
vuguvugu tu, sasa hao ndio wale kondoo
uliowaona wakichambuliwa katikati ya kondoo…Walipaswa waende na wale wengine
lakini kwa upumbavu wao wamebaki..
Ndugu hatupaswi kupoa kwa namna yoyote, hizi ni nyakati za
mwisho,kanisa hili tunaloishi, ndilo kanisa la mwisho lijulikanalo kama
Laodikia, Ndio lile la mwisho kati ya yale 7 yazungumziwayo katika kitabu cha
Ufunuo 2&3, Israeli imeshakuwa taifa huru tena, Ni nini tunachokisubiria sasa
kama sio UNYAKUO.
Na Bwana anasema Kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo
itakavyokuwa katika siku za kuja kwake mwana wa Adamu,.Ikiwa utautazama upepo
wa ulimwengu na kujifariji kwa mambo maovu yanayoendelea, ukidhani kuwa Bwana
anatumia ile kauli ya “wengi wape”.
Utajikuta unaingia katika gharika ya dhiki kuu, wakati wengi wapo mbinguni
kwenye karamu ya mwanakondoo. Ndugu Unyakuo hautakuwa wa wazi kama watu
wanavyodhani, unyakuo utakuwa ni SIRI, Na watakaofahamu ni wale wanawali
werevu, wachache sana. Lakini dunia nzima itakuwa buzy wakati huo kumfurahia
mpinga-Kristo na utawala wake.
Uamuzi ni wako ndugu unayesoma ujumbe huu, Kristo anarudi,
na wala hatakawia, atakusanya ngano ghalani mwake na magugu atayupa katika moto
usiozimika…Tubu dhambi sasa, ukabatizwe, na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu,
kwasababu hatuna wakati mwingi katika kizazi hichi.
Ubarikiwe.
No comments:
Post a Comment